Jumatano 21 Mei 2025 - 08:50
Iran ni miongoni mwa nchi 12 zenye mzunguko kamili wa teknolojia ya anga za mbali

Hawza/ Iran ikiwa na mzunguko kamili wa teknolojia ya anga za mbali, inahesabiwa kuwa miongoni mwa nchi 12 zinazoongoza duniani katika sekta hii

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika sekta ya teknolojia ya anga za mbali. Mafanikio haya ni ushahidi wa uwezo na weledi wa hali ya juu wa wanasayansi wa Iran katika fani hii.

Iran ni miongoni mwa nchi 12 duniani zenye mzunguko kamili wa teknolojia ya anga za mbali, na inajishughulisha katika nyanja za setilaiti, vituo vya ardhini, makombora ya kurushia satelaiti, pamoja na matumizi ya mitandao ya kisatelaiti.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha